FOUNTAIN GATE WANA BALAA ZITO

Klabu ya Fountain Gate ina balaa zito kwa kuzipoteza timu zote 15 Bongo katika eneo la utupiaji mabao ikiwa namba moja kwa safu kali ya ushambuliaji.

FOUNTAIN GATE WANA BALAA ZITO

Timu hiyo baada ya mechi 9 safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Suleman Mwalimu mwenye mabao sita ni mabao 19 imefunga kimiani msimu wa 2024/25.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Ikiwa ni namba moja kwenye eneo hilo namba mbili ni Simba ambayo safu yake ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 16 kibindoni huku Yanga na Singida Black Stars hizi mbili zote zimetupia mabao 13 kwenye mechi zao.

FOUNTAIN GATE WANA BALAA ZITO

Ikumbukwe kwamba mchezo wao uliopita Fountain Gate wakiwa nyumbani walipindua meza kibabe mbele ya Mashujaa ya Kigoma kwa kupata bao la jioni kupitia kwa kiungo Salum Kihimbwa ambaye alipiga faulo iliyozama mazima nyavuni.

Yanga ni namba moja kwa timu yenye ukuta mgumu ikiwa haijaruhusu bao la kufungwa ndani ya uwanja baada ya kucheza mechi 8.

Acha ujumbe