YANGA INA MAAJABU MENGI

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa timu hiyo ina maajabu mengi kutokana na kuwa kwenye ubora katika mechi zote pamoja na wachezaji wanaojituma muda wote.

YANGA INA MAAJABU MENGI

Ikumbukwe kwamba Yanga baada ya kucheza mechi 8 ndani ya ligi ambazo ni dakika 720 haijapoteza mchezo ikiwa imekomba pointi 24 nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Namba mbili ni Singida Black Stars ambayo ilipoteza kwenye mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0 na Young Africans Uwanja wa New Amaan Complex bao la ushindi likifungwa na Pacome dakika ya 67.

YANGA INA MAAJABU MENGI

Gamondi amesema kuwa wapo ambao wanaisema vibaya Young Africans kuhusu kiwango chake jambo ambalo halina ukweli kwani timu hiyo inacheza kwenye kiwango kizuri ikiwa na maajabu.

“Kuna maajabu mengi kuhusu klabu ya Wananchi hasa kwenye upande wa viwango, pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wanacheza kwa kujitum katika kutimiza majukumu hili ni muhimu na linapaswa kuwa endelevu.

“Yanga sio sawa na timu nyingine kwa namna ambavyo inacheza haimanishi kwamba hizo nyingine hazina ubora hapana hii sio kama Pamba Jiji pengine hii ni Yanga.”

Acha ujumbe