Manchester City Yaendelea Kuandamwa na Wimbi la Majeruhi

Klabu ya Manchester City bado inaendelea kuandamwa na jinamizi la majeruhi kwenye kikosi chao baada ya jana kuongeza mchezaji mwingine kwenye orodha ya wachezaji ambao wana majeraha baada ya winga Savinho kupata majeraha.

Winga Savinho raia wa kimataifa wa Brazil alishindwa kumaliza mchezo jana dhidi ya Tottenham Hotspurs ambapo waliishia kufungwa kwa mabao mawili kwa moja, Mchezaji huyo alionekana kuumia kwelikweli na kufanya kubebwa na machela ili kutolewa nje ya uwanja kitendo ambacho kiliacha maswali mengi kwa mashabiki wa Man City.manchester cityMpaka sasa madaktari wa klabu ya Man City hawajatoa taarifa kua winga Savinho atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini pia kocha Guardiola aliweka wazi kua wanasubiri ripoti ya madaktari ili kujua winga huyo wa kimataifa wa Brazil atakua nje ya uwanja kwa kipindi kirefu au kifupi.

Savinho ameungana wachezaji kama Rodri, Walker, Kevin de Bruyne, Grealish, pamoja na kinda Oscar Bobb katika orodha ya wachezaji majeruhi klabuni hapo, Manchester City msimu huu imepitia kipindi kigumu kwelikweli kwani wachezaji wake muhimu wamekua wakiandamwa na majeraha mfululizo.

Acha ujumbe