Manchester City Yapata Mkurugenzi Mpya wa Michezo

Klabu ya Manchester City itakua na mkurugenzi mpya wa michezo kuanzia mwezi Juni mwaka 2025 baada ya mkurugenzi wao wa michezoTxiki Begiristain kutangaza kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Txiki Begiristain ambaye amedumu ndani ya klabu ya Manchester City kwa takribani miaka 12 ambapo alijiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akifanya makubwa ndani ya timu hiyo na kuamua kutimka,Mabingwa hao watetezi wa Uingereza watakua na Hugo Viana kuanzia mwezi Juni 2025 kama mrithi wa Xiki.manchester cityHugo Viana raia wa kimataifa wa Ureno ambaye anaitumikia klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno atafanikiwa kujiunga na klabu hiyo ya nchini Uingereza kuanzia mwezi Juni mwakani, Huku makubaliano ya pande zote mbili yakifikiwa ya yeye kua mkurugenzi mpya wa michezo wa klabu ya Man City.

Hugo Viana atakua na mtihani mzito wa kuvaa viatu vya mkongwe Xiki Begiristain kwani gwiji huyo amefanikiwa kuhakikisha anashinda kila taji ndani ya klabu ya Manchester City na amefanikiwa katika hilo, Hivo Hugo Viana anatakiwa kuendeleza ambapo Xiki ameishia japo haitakua kazi rahisi ila ameaminiwa kutokana na uwezo wake na hiyo ikitokana na mazuri ambayo ameyafanya ndani ya Sporting Lisbon.

Acha ujumbe