Manchester City Yabanwa Mbavu na Newcastle

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City wamesare mchezo wa pili mfululizo kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja na Newcastle United.

Manchester City walifanikiwa kupata goli  kupitia kwa beki wake Josko Gvardiol mnamo dakika ya 35 ya mchezo na kufanikiwa kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa wanaongoza kwa goli moja kwa sifuri mbele ya wenyeji klabu ya Newcastle United ambao walikua wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.manchester cityKipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo klabu ya Newcastle United walionekana kuanza kwa kasi wakihitaji kusawazisha goli walilotanguliwa na City, Matarajio yao yalifanikiwa kwani dakika ya 58 walipata penati ilyowekwa kimiani na Anthony Gordon na kufanya matokeo yawe goli moja kwa moja.

Klabu ya Manchester City bado wanaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kukusanya alama 14 katika michezo 6 ambayo wamecheza, Ila wanaweza kukaa kileleni kwa muda mchache kama klabu ya Liverpool watashinda mchezo wao dhidi ya Wolves ambapo watakua na alama 15.

Acha ujumbe