Klabu ya Arsenal imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Leicester City dakika za jioni kabisa baada ya wageni hao kutaka kubisha katika mchezo huo ambao washika mitutu hao wa London walihitaji ushindi kwelikweli.
Arsenal walitangulia kupata magili mawili ndani ya kipindi cha kwanza kupitia kwa winga Gabriel Martinelli na Leandro Trossard, Ambapo iliwafanya vijana wa Mikel Arteta kwenda mapumziko wakiwa na uongozi wa mabao mawili lakini pia kua na asilimia kubwa za kushinda mchezo huo.Kipindi cha pili kilianza kwa Leicester City kuonekana wanatafuta goli la kusawazisha na mapema tu dakika ya 47 beki James Justin kufunga goli moja, Kabla ya beki huyohuyo kurudi kambani tena kwa kupachika bao la pili mnamo dakika ya 63 na kufanya ubao kusomeka mabao mawili kwa mawili na vijana.
Kocha Mikel Arteta na vijana wake ndipo matumbo yalipoanza kupata joto kwakua ilionekana kama wanaenda kupata sare ya pili mfululizo baada ya kusuluhu na Man City wikiendi iliyomalizika, Lakini mambo yalienda vizuri kwani kwenye dakika za nyongeza walifanikiwa kupata magoli mawili kupitia kwa Leandro Trossard na kufanya kuibuka na ushindi.Klabu ya Arsenal sasa wamefikisha alama 14 kwenye kwenye michezo sita ambayo wamecheza mpaka sasa wakiwa wamefanikiwa kushinda michezo minne huku wakisare michezo miwili sawa na klabu ya Manchester City, Mpaka sasa kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza washika mitutu kutoka London wanakamata nafasi ya pili.