Lavia Arejea Mazoezini Chelsea

Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji anayekipiga ndani ya klabu ya Chelsea Romeo Lavia inaelezwa amerejea kwenye kikosi cha klabu hiyo ambapo alikua anasumbuliwa na majeraha wiki kadhaa nyuma.

Lavia amekua akisumbuliwa na majeraha kwa wiki kadhaa nyuma na kumfanya kukosa baadhi ya michezo ndani ya kikosi hicho, Lakini kocha wa klabu hiyo Enzo Maresca amethibitisha kua mchezaji huyo amerejea kwenye kikosi cha timu hiyo na anatarajiwa kuanza kucheza kwenye michezo ya mbeleni.laviaBaada ya kurejea kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hivo ni wazi sasa wachezaji pekee walio kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambao wanasumbuliwa na majeraha ni nahodha wa timu hiyo Reece James, pamoja na Malo Gusto lakini wengine wote wako vizuri kwajili ya kuipambania nembo ya klabu hiyo.

Msimu uliomalizika klabu ya Chelsea ilikua ikiandamwa na majeraha sana na ikiwa moja ya klabu ambazo zilipata majeraha wengi, Msimu huu unaonekana kuanza vibaya kwa klabu hiyo ambapo washapata majeraha kama watatu sasa wa kikosi cha kwanza ikiwemo Lavia ambae msimu uliopita karibu wote aliukosa.

 

 

 

 

Acha ujumbe