Romeo Lavia Pancha Tena

Kiungo wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Ubelgiji Romeo Lavia atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Wolverhampton kutokana na majeraha.

Romeo Lavia ambaye alionekana kuanza msimu vizuri katika mchezo wa kwanza dhidi ya Manchester City licha ya klabu yake ya Chelsea kupoteza mchezo huo, Kiungo huyo alicheza vizuri lakini leo anakwenda kuukosa mchezo dhidi ya Wolves kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya misuli.romeo laviaKiungo huyo alikua akisumbuliwa na majeraha msimu uliomalizika yaliyomfanya kukosa karibia kipindi chote cha msimu kwakua alifanyiwa upasuaji wa goti, Lakini msimu huu akionekana kurejea vizuri ghafla anapata tena majeraha ambayo haijafahamika yatamueka nje kwa muda gani.

Klabu ya Chelsea imekua moja ya timu ambazo zimekua zikiendamwa na majeraha mara kwa mara na Romeo Lavia amekua moja ya wahanga wa majeraha hayo, Ni wazi kiungo huyo wa zamani wa Southhampton kukosekana kwake leo ni pengo kwa klabu ya Chelsea kutokana na kiwango alichokionesha katika mchezo wa kwanza wa ligi.

Acha ujumbe