Ademola Lookman Dili Lake la Kwenda PSG Kizungumkuti

Dili la winga wa wa kimataifa wa Nigeria Ademola Lookman kujiunga na klabu ya PSG inaelezwa huenda likafa kutokana na mabingwa hao wa ligi kuu ya Ufaransa kutokua tayari kulipa kiasi kilichohitajika.

Klabu ya PSG inaelezwa haipo tayari kutoa kiwango ambacho klabu ya Atalanta wamekihitaji kutoka kwao jambo ambalo linaweza kufanya dili la winga huyo wa Atalanta kufeli, Japokua mchezaji huyo ameshaonesha kila dalilia anataka kujiunga na klabu ya PSG mabingwa wa Ufaransa.ademola lookmanKlabu ya Atalanta wanahitaji kiwango kikubwa kama taarifa zinavyoeleza jambo ambalo PSG wameona sio thamani sahihi ya mchezaji husika, Kiwango cha pesa ambacho Atalanta wamekiulizia kwa PSG hakijawekwa wazi lakini kinaelezwa ni kikubwa na miamba hiyo kutoka nchini Ufaransa haipo tayari kutoa.

Winga Ademola Lookman amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya Atalanta jambo ambalo limefanya vilabu kadhaa kuvutiwa nae ikiwemo vilabu mbalimbali kutoka Saudia Arabia, Lakini kipaumbele cha mchezaji huyo ni klabu ya PSG mpaka sasa ili aweze kujiunga na kabu hiyo ni Atalanta washushe dau ambalo wameliweka ili PSG waweze kulipa.

Acha ujumbe