Ademola Lookman Awindwa Barani Ulaya

Nyota wa klabu ya Atalanta Ademola Lookman amekua moja ya wachezaji wanaozivutia klabu mbalimbali barani ulaya kutokana na ubora ambao amekua nao mchezaji huyo.

Staa huyo wa kimataifa wa Nigeria amekua kwenye kiwango bora sana tangu ajiunge na Atalanta akitokea klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani. Ademola Lookman amekua moja ya wachezaji muhimu sana chini ya kikosi cha kocha Gianni Piero Gasperini.ademola lookmanKiungo huyo ambaye amewahi kupita vilabu vya Fulham, Leicester City, na klabu ya Everton amekua kwenye wakati mzuri sana ndani ya klabu ya Atalanta, Kwani mpaka wakati huu amefanikiwa kufunga mabao 11 na pasi tatu za mabao ndani ya michezo 18 ndani ya klabu hiyo.

Ademola Lookman amekua kwenye ubora mkubwa sana ndani ya Atalanta na kufanya vilabu tofauti tofauti barani ulaya kuanza kumnyatia kutokana na uwezo ambao anauonesha ndani ya jezi ya Atalanta ndani ya ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A.ademola lookmanMchezaji Ademola Lookman ni wazi amekua kwenye kiwango bora ndani ya Atalanta pengine kuliko klabu yeyote ambayo amewahi kucheza nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria, Kwani kushiriki katika mchango wa mabao 14 katika michezo 18 tu sio jambo ambalo amewahi kulifanya katika vilabu vyote alivyowahi kupita.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.