Arteta Awania Kocha Bora Tena

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kocha bora wa mwezi ndani ya ligi kuu ya Uingereza. Kocha huyo amechaguliwa kuwania tuzo ya kocha bora wa mwezi Januari.

Kocha Arteta ametajwa kuwanbia tuzo hiyo sambamba na makocha kama Thomas Frank wa klabu ya Brentford, Roberto de Zerbi wa klabu ya Brighton, Unai Emery kutoka Aston Villa, pamoja Steve Cooper kutoka klabu ya Nottingham Forest.ArtetaMakocha hao watano wametajwa leo kuwania tuzo hiyo kutokana na ubora ambao makocha hao wameonesha katika kipindi cha mwezi Januari na kuwezesha timu zao kupata matokeo bora. Huku makocha wote waliotajwa kwenye orodha wakiwa na wastani mzuri wa matokeo ya ushindi ndani ya mwezi Januari.

Kocha Mikel Arteta yeye amefanikiwa kuendelea kuiweka timu yake kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza kwa kipindi kirefu, Na kocha huyo amefanikiwa kuiongoza Arsenal kucheza michezo mitatu ya ligi kuu na kushinda miwili huku akisuluhu mchezo mmoja ndani ya mwezi Januari.Mikel Arteta anaingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo mwezi Novemba na Disemba ambazo zilijumuishwa kwa pamoja na yeye kuibuka mshindi na sasa anafanikiwa tena kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo, Huku akiwa na nafasi kubwa pia ya kushinda.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.