Real Madrid Wenyeji Madrid Derby Leo

Klabu ya Real Madrid itakua mwenyeji katika mchezo wa Madrid Derby dhidi ya mahasimu wao klabu ya Atletico Madrid katika mchezo kombe la mfalme nchini Hispania utakaopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu.

Klabu ya Real Madrid leo watakua na mahasimu wao katika mchezo wa Copa de le Rey leo katika mchezo wa nusu fainali wa kombe hilo lenye heshima yake nchini Hispania, Huu ni mchezo wa pili ambao utakua unawakutanisha miamba hii ndani ya msimu huu.Real MadridMchezo wa nusu fainali unatarajiwa kua mchezo mzuri na wenye ushindani wa hali ya juu kwakua vilabu vyote vina ubora mkubwa kuanzia wachezaji mpaka kwenye benchi la ufundi wakiwa na makocha bora kabisa, Lakini pia upinzani wa jadi baina ya vilabu hivi pia unapelekea mchezo huu kua wenye mvuto mkubwa.

Real Madrid wataingia kifua mbele katika mchezo huu kwani wameshafanikiwa kuifunga klabu ya Atletico Madrid ndani ya msimu huu kwenye ligi kuu ya Hispania, Hivo inaweza kua faida kwa upande wao na kuingia kwa kujiamini lakini pia mahasimu wao wataingia kwa tahadhari na kutaka kuepuka uteja dhidi ya Los Blancos.Real MadridReal Madrid watakua na nyota wao wote katika mchezo wa leo dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo huo wa nusu fainali, Lakini wataendelea kukosa huduma ya kiungo fundi raia wa kimataifa wa Ufaransa Aurelien Tchouameni ambaye anauguza majeraha yake bado.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.