KOCHA VITAL 'O AKATA TAMAA KUIFUNGA YANGA

Kocha wa klabu ya Vital’O FC, Sahabo Parris amebainisha kuwa ni vigumu kuifunga Yanga SC mabao matano katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa barani Afrika.

Amesema kuwa kitu ambacho wanakwenda kufanya ni kuangalia kama hawatafungwa mabao manne tena katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex Chamanzi siku ya Jumamosi Agosti 24,2024.

Katika mchezo wa kwanza klabu ya Vital’O FC iliambulia kichapo cha mabao 4-0 na kujiweka katika wakati mgumu wa kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Acha ujumbe