Kevin de Bruyne Kuikosa Newcastle Kesho

Kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne anatarjiwa kuendelea kua nje ya uwanja zaidi ambapo kesho tena ataukosa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Newcastle United.

Kevin de Bruyne alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Inter Milan na kushindwa kumaliza mchezo huo, Ambapo ulipelekea kuukosa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Arsenal ambao ulipigwa wikiendi iliyomalizika na kesho anatarijiwa kuikosa Newcastle.kevin de bruyne“Kevin de Bruyne atakosa pia mechi dhidi ya Newcastle kwani Manchester City bado wanamfanyia tathmini.”

“Sijui ni lini atarudi. Labda kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa, au baada ya mapumziko ya kimataifa. Tutaona…”, amesema Pep Guardiola.

Klabu ya Manchester City inapitia kipindi kigumu kwasasa kwakua wachezaji wake muhimu wamepata majeraha haswa kwenye eneo la kiungo, Ambapo ukiachana na Kevin de Bruyne kiungo Rodri nae amepata majeraha ambayo yamemfanya msimu uliobakia aukose lakini KDB anatarajia kurejea uwanjani.

Acha ujumbe