Dumfries Aongeza Mkataba Inter Milan

Beki wa kimataifa wa Uholanzi Denzel Dumfries anayekipiga ndani ya klabu ya Inter Milan amefanikiwa kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2028.

Beki Dumfries mkataba wake ulikua unamalizika mwishoni mwa msimu huu kwa maana ya mwezi Juni mwaka 2025 lakini amefanikiwa kuongeza mkataba wa miaka mingine mitatu kuendelea kusalia kwenye viunga vya Milan ambapo amefanikiwa kupata mafaniko kama kucheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya na ubingwa ligi kuu ya Italia.dumfriesBeki huyo ambaye amejiunga na klabu ya Inter Milan mwezi Juni mwaka 2021 amekua na mwendelezo bora wa kiwango ndani ya timu hiyo chini ya kocha Simeone Inzaghi, Kitendo ambacho kimewavutia mabosi wa klabu hiyo kuendelea kuhitaji huduma yake ndani ya kikosi hicho.

Beki Dumfries kuna kipindi alikua akifuatiliwa kwa karibu na klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza lakini klabu ya Inter Milan haikua tayari kumuachia mchezaji huyo, Lakini pia mchezaji mwenyewe ameonesha anafurahishwa na maisha ndani ya klabu ya Inter Milan.

Acha ujumbe