Guardiola: Rodri Hatacheza tena Msimu huu

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amethibitisha kua kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Hispania Rodri haweza kucheza tena ndani ya msimu huu na atakua fiti msimu ujao.

Kiungo Rodri alipata majeraha ya goti katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi iliyopita dhidi ya klabu ya Arsenal na amefanyiwa upasuaji wiki, Hivo imethibitika mchezaji huyo hataweza kucheza msimu huu tena kwa michezo iliyobakia ili kua tayari kuitumikia klabu hiyo mpaka msimu ujao.guardiola“Kwa bahati mbaya, Rodri alipata matokeo mabaya zaidi.”

“Alifanyiwa upasuaji asubuhi ya leo, ACL na sehemu ya meniscus. Msimu huu umekwisha kwa Rodri.”

“Msimu ujao, atakuwa hapa.”

Klabu ya Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola ni wazi itapitia kipindi kigumu kutokana na kukosekana kwa kiungo Rodri ndani ya kikosi hicho, Kwani kiungo huyo kwa misimu mitatu sasa amekua mchezaji muhimu sana ndani ya kikosi cha mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza.

Acha ujumbe