Kevin De Bruyne Aweka Wazi Kuzitamani Hela za Saudia

Kiungo Kevin de Bruyne ameweka wazi kua yupo tayari kwenda kuzifata pesa nyingi ambazo zinatolewa kwenye ligi kuu ya Saudia Arabia maarufu kama Saudian Pro League.

“Saudi?Kwa  umri wangu unapaswa kua muwazi kwenye kila jambo,unaongelea kiwango kikubwa cha pesa kwenye nyakati zangu za mwisho kwenye mpira unapaswa kufikiria hilo”kevin de bruyne“Kama nitacheza Saudi kwa miaka miwili ninaweza kupata kiwango cha pesa ambacho nisingeweza kupata ningecheza soka kwa miaka 15 hapo nyuma”Alisema kiungo huyo wa Manchester City.kevin de bruyneKutokana na kauli ambayo ameitoa Kevin de Bruyne ni wazi kiungo huyo yuko tayari kutimkia Saudia kama watakuja na ofa ambayo itamvutia, Kwani ameweka wazi yupo kwenye nyakati za mwisho katika soka hivo ni wazi kukataa kiwango kikubwa cha pesa kinachotolewa Saudi kwakua huwezi kukipata sehemu nyingine.

 

Acha ujumbe