Mbappe: Niliambiwa Wazi Sitacheza Tena PSG

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Real Madrid Kylian Mbappe ameweka wazi kua uongozi wa juu wa klabu ya PSG ulimueleza wazi hatakwenda kucheza ndani ya timu hiyo mwanzoni mwa msimu ulioisha.

Mbappe ameeleza kua watu waliomsaidia yeye kucheza ndani ya timu hiyo ni mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Luis Ocampos, pamoja na kocha wasasa wa klabu hiyo Luis Enrique.mbappeNi wazi mshambuliaji huyo alipishana na uongozi wa juu wa klabu hiyo baada ya kugoma kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo, Hivo klabu hiyo ilitaka kumkomoa kwa kutomchezesha kabisa kwenye kikosi cha klabu hiyo.

Kutokana na taarifa aliyoitoa mchezaji huyo mpya wa Real Madrid ni wazi alipishana na Rais wa klabu hiyo Naseer Al Khelaif, Kwani waliomsaidia yeye kupata nafasi ya kucheza ni kocha wa klabu pamoja na mkurugenzi wa ufundi.mbappeMbappe alishaonesha msimamo wake toka mwanzoni mwa msimu ulioisha kua hataongeza mkataba ndani ya klabu ya PSG, Jambo linaelezwa halikuufurahisha uongozi wa juu wa klabu hiyo na kupelekea kutaka mchezaji huyo asicheze mpaka pale ambapo ataondoka bure mwishoni mwa msimu.

Acha ujumbe