TABORA UNITED KUKIPIGA NA JKT PLAY OFF LEO

Michezo ya PlayOff kwa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inaanza kutimua vumbi leo kwa mechi nne za kutafuta nani atacheza ligi kuu msimu ujao ambapo mchezo utakaoanza ni kati Tabora United dhidi ya JKT.

Play Off hiyo inahusisha jumla ya timu tatu, mbili kutoka Ligi Kuu na Moja kutoka Championship. Timu za Ligi Kuu ni zile zilizoshika nafasi ya 13 na 14 ambazo ni Tabora United na JKT Tanzania.tabora unitedHuku timu Moja ikiwa ni Biashara United kutoka Championship. Vita itaanza Kwa JKT na Tabora ambao watapambana Ili kutafuta nafasi ya kubaki Ligi Kuu Moja kwa Moja. Kwa kucheza mechi za Nyumbani na Ugenini na mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu.

Kisha atayepoteza atacheza mechi nyingine mbili na Biashara United, atakayeshinda kati ya Biashara na mmoja kati ya JKT Tanzania na Tabora United atapanda Ligi Kuu na atakayepoteza atabaki Championship.

Ratiba ipo hivi.

Tabora United vs JKT

JKT Tz vs Tabora United
08/06/2024 (2nd Leg)

Biashara Utd vs Tabora Utd/JKT Tz
12/06/2024 (Ist Leg)

Tabora United /JKT Tz vs Biashara Utd
16/06/2024 (2nd Leg)

Acha ujumbe