Kiungo mahiri wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne ameweka rekodi ndani ya klabu hiyo leo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Crystal Palace.
Kiungo huyo alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Palace, Huku yeye akifanikiwa kuweka rekodi kwani leo amefanikiwa kufikisha mabao 100 tangu ajiunge na klabu hiyo.Kevin De Bruyne amefanikiwa anafanikiwa kujiunga na wachezaji waliofunga mabao 100 ndani ya klabu hiyo, Wakiongozwa na mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo Serfio Aguero mwenye mabao 260 na Raheem Sterling mwenye mabao 130.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amefanikiwa kufikisha rekodi hiyo baada ya kucheza michezo 372 ndani ya kikosi cha Manchester City, Lakini mbali na mabao hayo 100 lakini pia amefanikiwa kupiga pasi 167 za mabao mpaka wakati huu.Kiungo Kevin De Bruyne mpaka sasa amefanikiwa kuhusika na mabao 267 tangu ajunge na klabu hiyo mwaka 2015, Akifanikiwa kua moja ya wachezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Man City lakini pia moja ya wachezaji bora kabisa ndani ya ligi kuu ya Uingereza.