Gavi Mbioni Kurejea

Kiungo wa klabu ya Barcelona Gavi inaelezwa yupo mbioni kurejea uwanjani baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwaka mzima kutokana na majeraha ya goti ambayo yalipelekea kufanyiwa upasuaji.

Gavi amekua nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake ya goti ambapo yalifanya kuacha pengo kubwa ndani ya klabu ya Barcelona msimu uliomalizika, Lakini taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania yupo mbioni kurejea kwenye timu hiyo na kuanza kuitumikia tena kama awali.gaviKiungo huyo ameshaanza kufanya mazoezi ya peke yake ndani ya timu hiyo na kuanza kufanya mazoezi kiwanjani lakini akiwa bado hajaanza kujumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi, Lakini timu ya madaktari ya klabu hiyo ipo mbioni kumruhusu aanze kufanya mazoezi ya pamoja na timu hii ikionesha atakua mbioni kuanza kuitumikia timu pia.

Wakati kiungo Gavi akitarajia kuanza mazoezi rasmi na wenzake ili aanze kuitumikia klabu yake klabu ya Barcelona wao wanafanya mazungumzo ya kumpa mkataba mpya wa muda mrefu kiungo huyo kwakua kiungo huyo ni sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu wa klabu hiyo, Taarifa zinaeleza kiungo pamoja na Pedri ni kipaumbele cha klabu ya Barcelona kwenye kuongezewa mkataba mpya ndani ya timu hiyo.

Acha ujumbe