Colwill: Nafurahi Kucheza Nafasi Yangu

Beki wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Uingereza Levi Colwill ameweka wazi kua msimu huu anafurahia zaidi kucheza nafasi yake ambayo amekua akiicheza kwa muda mrefu.

Colwill alikua akitumika kama beki wa pembeni msimu uliomalizika sehemu ambayo hakua anaifurahia kucheza japokua alipaswa kucheza na alikua tayari kwakua alikua anaisaidia timu yake, Lakini msimu huu anacheza nafasi ambayo ameizoea ambayo nafasi ya mlinzi wa katikati ambayo ndio nafasi anayopenda kucheza.colwill“Mwaka jana nilicheza katika nafasi ambayo si yangu kabisa na wakati mwingine nilijikuta kwenye changamoto… lakini mwaka huu najisikia kuwa na ujasiri zaidi.”

“Ninaweza kupiga pasi kwa Noni na kuonyesha uwezo wangu wa kupiga pasi kwa kiasi kikubwa zaidi.”

Beki Levi Colwill chini ya kocha Enzo Maresca amekua akitumika kama mlinzi wa kati ambapo ameoneha ubora mkubwa kama ambapo alikua akitumika kwenye klabu ya Brighton Hove and Albion sehemu aliyokua kwa mkopo, Nafasi ya mlinzi wa kati ndio nafasi ambayo beki huyo amekua akionesha ubora wake kwa kiwango kikubwa na kocha Maresca ameonesha imani kubwa kwa beki huyo.

Acha ujumbe