Man United Yamalizana na Amorim Mpaka 2027

Klabu ya Man United imefanikiwa kumalizana na kocha wa kimataifa wa Ureno Ruben Amorim ambaye alikua anaifundisha klabu ya Sporting CP mabingwa wa ligi kuu nchini Ureno ambapo atakua klabuni hapo mpaka 2027.

Baada ya kumfukuza kocha Erik Ten Hag raia wa kimataifa wa Uholanzi siku ya Jumatatu Man United walimpatia timu Ruud Van Nistelrooy aiongoze kwa muda, Huku wakiwa wanatafuta kocha wa kudumu ambapo walifanikiwa kumpata Ruben Amorim kutoka Sporting CP ambapo wamelipa kiasi cha Euro milioni 10 kwajili ya kumpata kocha huyo.man unitedTaarifa zinaeleza kocha huyo ataanza majukumu yake rasmi ndani ya klabu hiyo baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi Novemba, Huku mpaka sasa timu ikiwa chini ya kocha Ruud Van Nistelrooy ambaye ataiongoza timu hiyo kwenye michezo minne ambayo ni dhidi ya Leicester City kwenye Carabao ikiwa umeshachezwa, Chelsea, PAOK, na Leicester City kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Kocha Amorim anakuja ndani ya Man United pamoja na benchi lake la ufundi ambalo amekua akifanya nalo kazi ndani ya kikosi cha Sporting CP, Huku ikielezwa ndio sababu ya kuchelewa kujiunga na Man United kwakua walikua wanafanya mazungumzo juu benchi la ufundi la kocha huyo na hatakua kwenye benchi la klabu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Chelsea wikiendi hii kama taarifa zilivyoeleza awali.

Acha ujumbe