Amorim: Man United ndio Chaguo Langu

Kocha mpya wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ureno Ruben Amorim (39) ameweka wazi chaguo lake ilikua kujiunga na klabu hiyo mbali na kuhitajika na vilabu kadhaa barani ulaya.

Amorim ambaye amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi kuu ya Ureno na mpaka sasa akiwa anaongoza ligi hiyo kuonesha kwa namna gani amekua kwenye ubora na timu hiyo, Lakini maneno yamekua yakizungumzwa ni kua pesa ndio jambo limemng’oa ndani ya Sporting CP jambo ambalo amekanusha.amorim“Nimepokea maombi kutoka vilabu vingi katika miezi ya hivi karibuni… lakini klabu niliyotaka ilikuwa Manchester United”.

“Hakuna shabiki wa Sporting aliyependa nikae hadi mwisho wa msimu kuliko mimi. Lakini haikuwezekana.”

“Watu wengine wanasema nilijiunga na Man United kwa ajili ya pesa. Si hivyo.”

“Vilabu vingine vilikuwa tayari kulipa mara tatu zaidi na nilikataa… kwa sababu hiki ndicho klabu nilichotaka: Man United.” Alisema Amorim

Acha ujumbe