Staa wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Inter Miami Lionel Messi ameweka wazi kua hana mpango wa kuja kua kocha pindi ambapo atamaliza kucheza mpira wa miguu na kutangaza kustaafu.
Kumekua na wimbi kubwa la wachezaji ambao waliwahi kucheza mpira kusomea ukocha na baadae kua makocha jambo ambalo Messi yeye ameonesha kua sio kipaumbele chake, Hii inaendelea kuonesha utofauti wa staa huyo licha ya kua na kipaji cha kipekee lakini pia amekua wakipekee mara kwa mara katika maisha yake binafsi.
“Sipangi kua Meneja nitakapostaafu, Sio kitu ambacho ninakifikiria” Alinukuliwa staa huyo akizungumza na kuonesha kua kuja kua kocha wa mpira wa miguu sio mambo yake kabisa ambapo ni tofauti na wachezaji wengi ambao wakimaliza kucheza soka wanakua makocha wa vilabu mbalimbali.
Staa Lionel Messi ameamua kuchagua njia ya tofauti na wenzake labda yeye anatamani kua kiongozi wa timu na sio kocha kama mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Gerrard Pique ambaye inaelezwa kua beki huyo anataka kugombea nafasi ya Urais ndani ya klabu ya Barcelona.