Hansi Flick: Araujo Kurejea hivi Karibuni

Kocha wa klabu ya Barcelona Hansi Flick ameweka wazi beki wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uruguay Ronald Araujo anaendelea vizuri kwasasa, Hivo anaweza kurejea siku za hivi karibuni kuitumikia klabu hiyo.

Beki huyo ambaye alipata majeraha akiwa anaitumikia timu yake ya taifa ya Uruguay na kupata jeraha kubwa lilimfanya afanyiwe upasuaji ambao ulimfanya atarajiwe kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne, Lakini taarifa zinaeleza kua beki huyo anaweza kurejea mapema tofauti na ilivyotarajiwa.flickAraújo yuko katika hali nzuri, hatutamharakisha kurudi.”

“Lazima tumwangalie kwa makini kwani anarudi baada ya jeraha baya. Nitafurahi atakaporudi kuwa nasi.”

Beki Ronald Araujo amekua moja ya wachezaji muhimu kwa misimu mitatu sasa ndani ya kikosi cha Barcelona jambo ambalo litaifanya klabu hiyo kufurahia urejeo wake kikosini na ni taarifa nzuri kwa kocha Hansi Flick, Haswa wakati huu ambao timu hiyo inafanya vizuri lakini pia inashiriki michuano mingi hivo ni muhimu kua na wachezaji wengi wenye ubora kikosini.

Acha ujumbe