Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Hans Flick amesema hajawagi kufikiria kujiuzulu kuifundisha timu hiyo baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Timu ya taifa ya Ujerumani ilitolewa mapema kwenye hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Huku ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa timu hiyo kutolewa kwenye hatua hiyo baada ya kufanya hivo mwaka 2018.hans flickKocha Hans Flick anasema ana mawasiliano mazuri na viongozi wa soka la Ujerumani hivo kujiuzulu nafasi hiyo haikuwahi kua kipaumbele chake, Na zaidi anameweka mipango zaidi kwenye michuano ambayo ipo mbeleni.

Hans Flick amesema kwenye michezo ya kombe la dunia walikosa mwendelezo bora wa kiwango kwa dakika 90 za mchezo, Lakini ni kitu ambacho amepanga kukitengeneza kwa timu yake katika siku zijazo kwajili ya michuano mingine mikubwa.hans flickUjerumani ndio wenyeji wa michuano ya kombe la Euro mwaka 2024, Hivo watahitaji kuandaa timu ambayo itakua na ushindani kuelekea michuano hiyo ambayo itafanyika kwenye ardhi yao ya nyumbani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa