Timu ya taifa ya Croatia imefanikiwa kuibuka mshindi wa tatu kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga timu ya taifa ya Morocco kwenye mchezo wa mshindi wa tatu uliopigwa katika dimba la Khalifa International.

Mabao ya Josko Gvardiol na Mislav Orsic yaliifanya timu ya taifa ya Croatia kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja, Huku bao la kufutia machozi la timu ya taifa ya Morocco likiwekwa kimiani na beki Achraf Dari.CroatiaTimu ya taifa ya Croatia ambayo imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali mfululizo mara ya kwanza kwenye historia ya nchi hiyo baada ya kufanya hivo mwaka 2018 ambapo walikua washindi wapili na leo wamefanikiwa kua washindi watatu.

Timu hiyo chini ya kocha Zlatko Dalic imefanikiwa kua na mafanikio makubwa baada ya kucheza fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 na mwaka 2022 kufanikiwa kumaliza kama washindi watatu, Haya yamekua mafanikio makubwa kwa kocha huyo pamoja na timu kwa ujumla kwakua wamekua hawapewi nafasi lakini wanafanya vizuri.croatiaTimu ya taifa ya Croatia imekabidhiwa medali zao za mshindi wa tatu na rais wa shirikisho la mpira duniani Gianni Infantino punde baada ya kuifunga timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa mshindi wa tatu wa kombe la dunia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa