Golikipa wa timu ya taifa ya Argentina Emiliano Martinez amesema kua nahodha wa timu hiyo Lionel Messi anawapa faida zaidi ya kushinda mchezo wa fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Lionel Messi atacheza mchezo wa fainali wa jumapili dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa na atakua anaweka rekodi kama mchezaji aliecheza michezo mingi kwenye michuano hiyo akiwa amefikisha michezo 26.martinezLionel Messi amekua kwenye kiwango bora sana kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kuisaidia timu yake kutinga fainali ya michuano hiyo, Huku akiwa anaongoza kua mchezaji mwenye mchango mkubwa wa mabao akiwa amefunga mabao matatu na kupiga pasi tatu za mabao hiivo mchango wake ni mabao 8.

Kipa Martinez anasema kuwepo kwa Messi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kunawapa nguvu wachezaji wote wa kikosi hichi kwasababu wana mchezaji bora duniani kwenye kikosi chao kitu ambacho kinawapa faida.martinezEmiliano Martinez ambaye amekua kwenye ubora mkubwa kwenye michuano hii amesema anajua watu wengi watawapa nafasi zaidi timu ya taifa ya Ufaransa, Lakini wao wana mchezaji anaeweza kufanya vitu vya ziada na kuwapa faida zaidi wao ambaye si mwingine ni Lionel Messi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa