Pogba Hana Mpango wa Kurejea Man United

Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba ameweka wazi hana matamanio ya kurejea ndani ya klabu hiyo siku moja baada ya kutimka mwezi Juni mwaka 2022.

Kiungo Paul Pogba amezungumza mambo mengi baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu takribani mwaka mmoja ambapo aliulizwa na kama anaikumbuka na kutamani labda kurejea siku moja ndani ya viunga vya Old Trafford na majibu yake yalionesha kua hana mpango wa kurejea ndani ya klabu hiyo.pogba“Ninaangalia Manchester United! Bado nina wachezaji wenzangu pale. Bado ni moja ya vilabu vikubwa zaidi duniani.”

“Lakini sikuwa nafikiria mambo mengine zaidi.”

Kiungo Paul Pogba pamoja na kueleza kua hana mpango wa kurejea ndani ya klabu ya Man United na ikihusishwa na vilabu kadhaa baada ya kutoka kifungoni ambapo alifungiwa kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu mchezoni, Ameeleza yupo tayari hata kupunguziwa mshahara ili aendelee kuitumikia Juventus kwakua anajiona ni mwenye deni klabuni hapo na anapaswa kulilipa.

Acha ujumbe