Luis Enrique Kujifunga PSG

Kocha Luis Enrique anakaribia kumwaga wino wa kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu ya PSG mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa ambao amejiunga nao mwaka 2023 mwezi Juni.

Luis Enrique alijiunga na timu hiyo baada ya kuachana na kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Hispania baada ya michuano ya kombe la dunia kule nchini Qatar, Kocha huyo anaonekana kuvutiwa na mipango ya mabingwa hao wa Ufaransa siku za usoni na ndio sababu ya kukubali kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo.luis enriqueKocha huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kusaini mkataba mpya ambao uataendelea kumuweka ndani ya PSG mpaka mwaka 2027,kocha huyo anaelezwa tayari ameshakubaliana kila kitu na uongozi wa klabu hiyo na kinachosubiriwa kwasasa ni kumwaga wino kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Parc de Princes.

Kocha Luis Enrique tayari ameshafanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Ufaransa lakini ndoto kubwa ya klabu hiyo na yeye pia ni kuhakikisha anaisaidia klabu hiyo kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya kama ambavyo alifanya na klabu ya Barcelona mwaka 2015, Kwani ligi kuu ya Ufaransa wametwaa makocha wengi lakini kipaumbele cha klabu hiyo ni taji la ulaya.

Acha ujumbe