Luis Enrique Atua PSG

Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Luis Enrique raia wa kimataifa wa Hispania amefanikiwa kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya PSG kwa mkataba wa miaka miwili.

Baada ya klabu ya PSG kumvunjia mkataba aliyekua kocha wake Christopher Galtier wakafikia maamuzi ya kumpatia mkataba wa miaka miwili kocha Luis Enrique ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2025.Luis EnriquePSG wamekua hawadumu na mamocha kwa muda mrefu ndani ya timu hiyo na hiyo inaelezwa ni moja ya sababu ya kumpa kocha huyo mkataba wa miaka miwili tu, Kwani mara nyingi wanaposainisha makocha mikataba ya muda mrefu na kuja kuwafukuza hua inawapa hasara kwani wanahitajika kulipa fidia.

Luis Enrique baada ya kutambulishwa ndani ya klabu ya PSG raia wa klabu hiyo Nasser Al-Khelafi ameendelea kusisitiza kua hawako tayari kumuachia mchezaji huyo bure mwaka 2024 na kusema msimamo wao ni wamuuze mchezaji huyo sasa au asaini mkataba mpya.Luis EnriqueKocha Luis Enrique ameletwa ndani ya PSG kwajili ya kuhakikisha klabu hiyo inafanya vizuri haswa kwenye ligi ya mabingwa ulaya ambapo wamekua wakichechemea ndani ya misimu miwili mfululizo wakitoka hatua ya 16 bora ambayo sio hatua nzuri kwa klabu kama PSG.

Acha ujumbe