Luis Enrique: Mbioni Kutua Chelsea

Kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique inaelezwa ametua ndani ya jiji la London kwajili ya kufanya mazungumzo na klabu ya Chelsea ili kuchukua kibarua cha kuionoa tiimu hiyo.

Luis Enrique ambaye mara ya mwisho ameiongoza timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Klabu ya Chelsea kwasasa ipo kwenye mpango wa kuajiri mwalimu mpya baada ya kumfukuza aliekua kocha wa hiyo timu Graham Potter mwishoni mwa wiki iliyopita.Luis EnriqueKocha huyo wa kimataifa wa Hispania amekua moja ya kocha anaivutia klabu ya Chelsea kipindi hichi ambacho timu hiyo inatafuta kocha mpya, Huku taarifa zikieleza kua kocha huyo jijini London kwajili ya kuzungumza na klabu ya Chelsea kwajili ya kuchukua kibarua hicho.

Luis Enrique inaelezwa kua kwa asilimia 100 amevutiwa na kazi ya kuinoa klabu ya Chelsea hivo kama mazungumzo yatakwenda vizuri baina ya klabu hiyo dhidi ya kocha huyo ni wazi kocha huyo atachukua mikoba ya aliekua kocha wa klabu hiyo Graham Potter.Luis EnriqueKocha Luis Enrique aliripotiwa kuikataa kazi ya klabu ya Tottenham Hotspurs baada ya kumfukuza mwalimu Antonio Conte, Lakini inafahamika kua kocha huyo anataka kufanya kazi Uingereza hivo ilipojitokeza fursa ya kibarua cha klabu ya Chelsea kocha huyo anaona kama ni sehemu sahihi kwake kufanya kazi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.