Luis Enrique Anaitamani Epl lakini sio Spurs

Kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique inaelezwa anavutiwa na kufundisha katika ligi kuu ya Uingereza lakini inaelezwa amekigomea kibarua cha kufundisha klabu ya Tottenham Hotspurs.

Klabu ya Tottenham Hotspurs inaelezwa ilikua inahitaji huduma ya kocha Luis Enrique baada ya kuachana na kocha wake raia wa kimataifa wa Italia Antonio Conte, Lakini kocha wa huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona amekigomea kibarua cha klabu hiyo.Luis EnriqueKocha huyo wa kimataifa wa Hispania amekua kwenye rada za timu mbalimbali za ligi kuu ya Uingereza kwa kipindi kirefu ikiwemo Manchester United ambayo tayari imeshapata kocha kwasasa ambaye anafanya vizuri, Lakini kocha huyo kwasasa licha ya kuvutiwa na ligi kuu ya Uingereza atalazimika kusubiri kibarua kwenye timu kubwa baada ya kuikataa kazi ya Spurs.

Luis Enrique amekua kocha wa viwango kwa muda mrefu sasa akihudumia klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania kwa mafanikio makubwa, Hivo kufanya kua moja ya makocha wa heshima kubwa barani ulaya na wenye kuwindwa zaidi kutokana na ubora wake.Luis EnriqueBaada ya kocha Luis Enrique kukataa kibarua cha kuitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs ambaye imemuondoa kocha Antonio Conte aliyekua akifundisha timu hiyo, Kocha Lucho sasa atahitajika kuangalia timu nyingine ndani ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kukigomea kibarua cha klabu ya Tottenham kama taarifa zinavyoeleza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.