Ten Hag: Weghorst Anafanya Kazi Kubwa

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema mshambuliaji wake ndani ya klabu hiyo Wout Weghorst anafanya kazi kubwa mpaka sasa na anachokifanya kinaleta mafanikio kwenye timu.

Kocha Ten Hag amesema kua tuhuma na lawama ambazo anatumiwa mchezaji huyo anaziona lakini yeye anaona mchezaji huyo amefanya kazi kubwa mpaka sasa kwenye timu hiyo, Huku akisema kuna ushahidi unaoonesha kua mchezaji huyo amefanya kazi kubwa ndani ya timu hiyo.Ten HagMshambuliaji Wout Weghorst amekua akitupiwa lawama na wadau mbalimbali kutokana na kiwango ambacho amekua akionesha ndani ya timu hiyo, Lakini kocha Ten Hag anaamini mchezaji huyo amekua na mchango mkubwa kwenye timu hiyo tangu amejiunga nayo.

Wout Weghorst amekua akionekana akichangia zaidi kuipa nguvu timu hiyo kwenye kuzuia zaidi tofauti na ambacho kilitarajiwa kutoka kwake, Huku mpaka sasa akiwa amefanikiwa kufunga mabao mawili tu vilevile akiwa hajafanikiwa kufunga bao kwenye ligi kuu ya Uingereza.Ten HagKocha Ten Hag pamoja na yote ambayo yanazungumzwa kumhusu mshambuliaji wake huyo alietoka kwa mkopo kutoka klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki anasema kua anafurahishwa na mwenendo wa mchezaji huyo, Pia akisema kiwango anachokionesha mpaka sasa kinaisaidia timu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.