Nabi Amuweka Gamondi Kitimoto

UNAAMBIWA pamoja na Kocha Mkuu wa Yanga kutua na wasaidizi wake, uongozi wa klabu hiyo umempatia masharti magumu msimu ujao ambapo imemtaka, kuhakikisha anachukua makombe yote ya ndani na kuifikisha timu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na akiyakosa basi alete Kombe la Shirikisho Afrika Huku Nabi akitajwa kama sababu.

Juni 24, mwaka huu ndiyo siku alipotambulishwa rasmi Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina kurithi mikoba ya Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambaye amemaliza mkataba na kusepa zake.NabiChanzo chetu makini kutoka ndani ya Yanga, kilisema, baada ya kocha kutoa mapendekezo yake na kupokelewa na uongozi, hatimaye na yeye ametakiwa kuhakikisha anaifikisha timu hatua ya Robo Fainali ya Caf na akishindwa basi alete Kombe la Shirikisho Afrika kama ambavyo alifanya kocha aliepita Nassrdine Nabi.

“Ukisikia mipango yetu ya mwaka huu, basi aminini kuwa malengo ya viongozi yako mbali sana na mawazo ya mashabiki, kwanza kocha atatakiwa kuhakikisha anabeba makombe yote ya ndani.

“Kisha ahakikishe anaifikisha timu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kama siyo ahakikishe anabeba Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kutokana na umahiri wake Gamondi amekubali hilo na amewahakikishia kufika mbali zaidi ya malengo yao ambapo ameomba uongozi kumpatia mahitaji yote ya benchi lake kwa wakati.Nabi“Ikiwemo suala la usajili kumalizika mapema ambapo tayari wachezaji wote aliowataka wameshasaini mikataba mipya,” kilisema chanzo hicho.

Hivi karibuni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa: “Tayari suala la usajili limeshakamilika na kwamba wachezaji wote wameshasaini mikataba na kilichobaki ni kuingia kambi na kungoja makombe ya msimu ujao.”

Acha ujumbe