Beki wa kati wa FC Barcelona Eric Garcia amekubali kuwa timu yake ilifanya makosa mengi ambayo hayakutakiwa kufanywa na kupelekea timu hiyo kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Inter Milan walipokuwa nyumbani hapo jana kwenye mchezo wa marudiano.

Mchezo wa kwanza Barca alipoteza kwa bao 1-0, na kwasasa kikosi hicho kinachoongozwa na kipo nafasi ya tatu ambayo si nzuri inayomtaka ashinde mechi zake mbili zilizobaki huku akiomba wa juu yake wapoteze mechi zao zote, kitu ambacho ni ngumu kwakweli.
Endapo Barca hawataweza kushinda mechi hizo atashuka na kwenda kushiriki michuano ya Uropa ambayo hushiriki timu zilizoshindwa kufuzu kwenye makundi na kwenda 16 bora.
Garcia na Barca walikuwa na deni la mabao mawili ya dakika za lala salama kutoka kwa Robert Lewandowski, ambaye alifuta bao la Robin Gosens dakika ya 89 baada ya kufanya matokeo kuwa 2-2.

Garcia alikiri kwamba Barca hawakuwa na matokeo mazuri katika kipindi cha pili ambapo pia Nicolo Barella na Lautaro Martinez walifunga baada ya bao la mapema la Ousmane Dembele.
“Tumefanya makosa ambayo hayawezi kufanywa katika kiwango hiki,” beki huyo wa kati aliiambia Movistar. “Tulikuwa pale tunapotaka, tukipiga mpira wa juu, tukiiba mipira na tulitaka kuendelea hivyo hivyo, lakini katika kipindi cha pili kulikuwa na upungufu mkubwa wa udhibiti na tulichukua hatari ya kucheza na watatu nyuma.
Kikosi cha Simone Inzaghi kinahitaji ushindi mmoja pekee kutoka katika mechi dhidi ya Viktoria Plzen na Bayern Munich, ambao tayari wamesonga mbele, ili kutinga hatua ya 16 bora – lakini mfungaji wa mabao Barella alisisitiza kuwa kazi bado haijakamilika.
“Tulitaka ushindi, Sare ilikuja badala yake, lakini bado tuna furaha sana na ari yetu uwanjani,” mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia aliiambia Amazon Prime Video. “Tunaipata na tumeridhika.

Baada ya mchezo huo, wikiendi hii Eric Garcia na wenzake wakuwa dimbani kucheza El Classico dhidi ya wapinzani wao wakuu Real Madrid huku mshindi kati yao ataongoza ligi kwa pointi.

