Gerard Pique : Shakira Ndio Mafanikio Yangu Makubwa Katika Soka.


Staa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Gerard Piqué Bernabeu, 34 ameelezea jinsi alivyokutana na mkewe Shakira Isabel Mebarak Ripoll, 44 ambaye ni msanii.

“Mara yangu ya kwanza kukutana na Shakira nilikuwa Madrid wakati tulikuwa tukifanya video ya ‘Waka Waka’ kabla ya Kombe la Dunia la 2010 na hapo ndipo niliomba namba yake. “alisema Pique

 

“Baadaye Shakira alikwenda Afrika Kusini kabla yetu (timu ya taifa ya Spain) wakati alikuwa akiimba kwenye sherehe ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia. Nilimtumia ujumbe kwenye simu na kumuuliza hali ya hewa ilikuwaje kwa sababu tulikuwa tunatarajia kufika Afrika Kusini katika siku chache.

“Hili ni swali la kawaida la kijinga unaloandika na kawaida hupata jibu kama ‘Ni baridi, njoo na koti’. Lakini haikuwa hivo aliandika ujumbe marefu, akielezea mabadiliko ya hali ya hewa jinsi kulivyo na joto siku nzima.

“Nilifikiria nikasema ‘Yesu, hii sio kawaida’. Ilikuwa katika maelezo yake hayo ambapo niliweza kusema kulikuwa na kupendana kati yetu. Tulianza kutumian ujumbe wakati wote wa mashindano ya World Cup.

 

“Lakini, nafasi pekee ambayo nilikuwa nayo ya kumuona ilikuwa kama tungefika hatua ya fainali, kwani wakati huo alikuwa na ratiba ya kutumbuiza kwenye sherehe ya kufunga fainali za dunia. Nilimwambia kwamba kama njia ya kumuona ni hadi siku ya Fainali, basi nitafanya hivyo.

“Mungu mwema tukafika hadi Fainali, ilikuwa jambo nzuri zaidi ambalo nilikuwa nimelipata tangu Spain tushinde Kombe la Dunia na hakika nikafanikiwa kukutana na mpenzi ymwa maisha yangu. Niliondoka Afrika Kusini nikiwa mtu mwingine kabisa. ” aliongeza Gerard Pique.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

11 Komentara

    Jambo jema sana

    Jibu

    Inapendeza 👏

    Jibu

    Ulitumia mbinu nyingi sana hadi kumnasa kimapenzi hongera san

    Jibu

    Behind the successful man there is women

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Kulikuwa na mapenzi ndani yao. Ndoa ya mfano

    Jibu

    Jambo zuri ongera yake

    Jibu

    Inafurahisha

    Jibu

    Raha sana

    Jibu

    Hadi raha

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

Acha ujumbe