Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Didier da Rosa Gomes, ameongelea swala kiungo mkata umeme, Jonas Mkude na ubora wake na jinsi gani anaweza kurejea katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

“Mkude namuamini na naamini katika uwezo wake na kipaji, lakini ili uweze kufikia malengo unatakiwa kutumia muda mwingi kufanya mazoezi utafika mbali zaidi ya hapa ulipo sasa, kama amenielewa na kukubaliana na kauli yangu nina imani atakuwa bora na ataisaidia Simba,” anasema Gomes
“Suala la kucheza kwenye kikosi cha Simba bado lipo kwenye mikono yake yeye mwenyewe Mkude,Lwanga (Tadeo), Sadio (Kanoute), Mzamiru (Yassin) na Erasto (Nyoni) wote ni wazuri kwenye kiungo lakini kila moja ana staili yake ya kucheza.”
“Kila mchezaji nimewahi kumpa nafasi ya kucheza hii inaonyesha nilikuwa naelewa umuhimu wao kikosini, shida ni kwa Mkude ambaye sijamtumia mara nyingi hivi karibuni kwasababu hajafanya mazoezi na timu muda mrefu,”
“Hakuna mchezaji ambaye hakuwa na namba kwenye kikosi changu, ukiona mchezaji sijamtumia basi kashindwa kunishawishi mazoezini na amekosa moja ya programu zangu kuelekea mchezo husika.” aliongeza Gomes.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

CHEZA HAPA

