Roberto Firmino amerejea kwenye kiwango chake msimu huu hali iliyopelekea kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp kumpa sifa kedekede akaenda mbali zaidi na kusema kwamba siku moja wataandika kitabu kuhusu staa huyo wa Brazil akicheza false 9 yaani namba tisa ya bandia na kuwatesa mabeki wa timu pinzani.

Katika michezo tisa ya Liverpool Firmino amefunga mabao sita na kutoa asisti moja na alikuwa mhcezaji mwiba katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Manchester United akiwatesa Victor Lindelof na Harry Maguire kwa kuzunguka na mpira.
“Bobby alicheza vyema kwa mara nyingine,” alimulezea katika mkutano na wandishi wa habari.
“Nina uhakika watu wataandika kitabu chake jinsi anavyo itendea haki namba tisa bandia.
Firmino amekuwa akicheza vizuri katika utatu wa Liverpool tangu zama Klopp huko Merseyside ingawa muda mwingine huwa hapewi sifa zake anazostahili amefanikiwa kufunga mabao 70 nyuma ya Sadio Mane mabao 90 na Mohammed Salah mabao 140.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

CHEZA HAPA

