Winga wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ambaye amekua nje ya kiwanja kwa takribani mwaka mmoja na nusu ameonekana kiwanjani kwa mara ya kwanza.
Greenwood jana ameshuhudiwa akiwa kiwanjani akifanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu akumbane na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia mwishoni mwa mwaka 2021 ambapo amekua nje ya uwanja mpaka leo hii.Winga huyo ameonekana kiwanjani jana ikiwa ni baada ya klabu ya Manchester United kutangaza kikosi ambacho kitabakia msimu ujao kwenye timu hiyo ambapo kiliwekwa wazi wiki moja iliyomalizika.
Mason Greenwood hakuwahi kuonekana akifanya mazoezi kiwanjani na sehemu ya wazi lakini jana mchezaji huyo ameonekana, Hii imeibua matumaini makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo wakiamini nyota huyo atakua sehemu ya timu hiyo msimu ujao.Winga Greenwood alikua na wakati mzuri sana ndani ya klabu ya Manchester United kabla ya kukumbana na shutuma zilizomueka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu, Lakini kuna taa ya kijani mpaka sasa inaonesha kua huenda mchezaji huyo akarejea kwenye timu.