Hatma ya Harry Kane kujulikana leo

Hatma ya mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane kujulikana leo ikiwa ndio siku ya mwisho ya mazungumzo.

Mshambuliaji Harry Kane anahitajika na klabu ya Bayern Munich kwa karibu zaidi ambao wameshatuma ofa mara mbili ndani ya klabu ya Spurs,Leo ikiwa siku ya mwisho ya kujua hatma ya mshambuliaji huyo lakini maamuzi yanatarajiwa kutoka kwa Mwenyekiti Danile Levy.harry kaneMwenyekiti Daniel Levy ndio anasubiriwa kuangalia atakua na maamuzi gani juu ya mshambuliaji huyo,Kwani kama atakataa ofa ya Bayern na ataamua mchezaji huyo kubaki ndani ya klabu hiyo itakua ngumu kwa Bayern kumpata mshambuliaji huyo.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza ameshaonesha nia ya yeye kuondoka ndani ya klabu hiyo, Lakini Spurs ndio wamekua wakiweka ugumu wa mchezaji huyo kutimka ndani ya klabu hiyo.harry kaneKlabu ya Tottenham chini ya mwenyekiti Daniel Levy ndio wanaweza kutoa mwanga kwa mshambuliaji Harry Kane leo kama watakubali ofa iliyotumwa na mabingwa wa soka kutoka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich basi mchezaji huyo atatimka klabuni hapo.

Acha ujumbe