Hazard Nje Mechi ya El Clasico.


 

Meneja wa Real Madrid amesema winger, Eden Hazard atakosekana kwenye mchezo wa leo wa El Classico dhidi ya Barcelona kutokana na kutofanya mazoezi ya kutosha na kikosi cha kwanza.

Zinedine Zidane alionya katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi, Eden Hazard hajarudi kwa wakati ili kujumuishwa katika kikosi cha Real Madrid kwa mchezo wa El Classico.

 

Mbelgiji huyo amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wenzake katika siku chache zilizopita, lakini bado haijatosha kumjumuisha kikosini. Matumaini ni kwamba Hazard atarudi katika hali thabiti ikiwa atajiimarisha na kuwa mkali kupitia vipindi vya mazoezi.

Kwa hivyo, hakuna mshangao mkubwa katika orodha ya kikosi cha Real Madrid. Labda jambo pekee la kuzingatia ni kukosekana kwa Sergio Arribas, ambaye mara kwa mara amehusika katika kikosi lakini badala yake atapata nafasi ya kucheza na timu ndogo ya Castilla kwa Raul Gonzalez wikendi hii.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Hatari sana

    Jibu

    Majanga

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

Acha ujumbe