Baada ya wamiliki wa timu ya Inter Milan kuonyesha dalili za kutaka kumuuza mshambuliaji wa timu hiyo, Romelu Lukaku kwaajili ya kubalance daftari la mahesabu la klabu hiyo mashabiki wameingilia kati.

Raisi wa Inter Milan, Steven Zhang alitaka kuuteka ulimwengu wa soka akiwa na Milan. Lakini sasa inaonekana klabu hiyo inataka kuanguka mikononi mwake.
Miezi mitatu tu baada ya taji la kwanza la Serie A la Inter baada ya miaka 11, rais wa klabu anapigiwa kelele na mashabiki kwa kuzingatia kumuuza mshambuliaji wao Romelu Lukaku.
Kumbuka, Nerazzurri, tayari wamempoteza meneja wao Antonio Conte, na beki bora wa kulia msimu uliopita, Achraf Hakimi, tangu walipotwaa Scudetto.
Mashabiki wanaamini, kitendo cha Raisi wa klabu hiyo kukubali zabuni ya Chelsea kumnunua mchezji huyo itakuwa ni kitendo cha usaliti.
Katika bango lililofunguliwa nje ya makao makuu ya klabu mnamo Jumatano, ‘Curva Nord’ yalionya wamiliki kwamba “Ahadi lazima zitimizwe”. Ilikuwa tishio dhahiri.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sania+mapua
Mashabiki wana msimamo thabiti