Kocha mkuu wa Intermilan Simone Inzaghi amesema kuwa hakuwa na wasiwasi kamwe kuhusu mchezaji wake Lautaro Martinez kwenye kufunga mabao ambapo aliingia kambani mara mbili hapo jana na kutoa pasi ya bao.

Mshambuliaji huyo wa Argentina aliiandikia Inter mabao mawili hapo jana kwenye mchezo walipokuwa ugenini dhidi ya Fiorentina uliomalizika kwa wao kushinda kwa mabao 4-3 na kuchangia pasi moja ya bao.
Martinez alikuwa ndiye chachu ya bao la ufunguzi la Nicolo Barella, lililofungwa dakika ya pili ya kuanza mchezo na dakika ya 15 wakaongeza bao lingine la pili kabla ya Fiorentina kuja kupata bao moja baadae na kwenda mapumziko ubao ukisomeka 2-1.
Mabao mawili ya Martinez yalifikisha jumla ya mabao yake 6 katika Serie A msimu huu na kumfanya awe juu pamoja kwenye orodha ya wafungaji, na Inzaghi alisema hakuwahi kuwa na wasiwasi wowote kuhusu ukosefu wa mabao wa mchezaji huyo wa miaka 25.
“Sikuwa na wasiwasi kuhusu Lautaro hata alipokuwa hafungi, kwa sababu huwa anafanya kile anachopaswa kufanya mazoezini na kwenye mchezo, zaidi ya malengo,” aliambia Gazzetta dello Sport.

Bosi wa Inter pia alimuunga mkono Joaquin Correa, ambaye aliona kujituma kwake huku mapambano yakiendelea na maonyesho yake huko Florence, na kuongeza kuwa Correa alikuwa vizuri usiku wa leo katika huduma ya timu na nafasi nzuri na Lautaro.
Inter pia wanatazamiwa kuongezwa nguvu kutokana na kurejea kwa wachezaji wake muhimu kutoka kwenye majeraha, huku Romelu Lukaku, Marcelo Brozovic na Roberto Gagliardini wakitarajiwa kurejea kwenye vita pia.
Inzaghi alisema kuwa hawawezi kusubiri kwasababu hajaweza kuwa nao kwenye mechi hizo, Lukaku, Brozovic na Gagliardini watarejea na tunawahitaji na hayo aliyasema baada ya kuona timu yake ikirejea juu kwenye nafasi ya 7 na kuipita Juventus kwenye nafasi ya 8.

Mechi inayofuata ni ya Ligi ya Mabingwa Inzaghi na vijana wake wanamenyana dhidi ya Viktoria Plizen wakiwa nyumbani huku Viktoria wakiwa hawajashinda hata mchezo mmoja kwenye kundi C. Inter wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 7 hivyo mchezo huo ni muhimu kwao.

