Aliyekuwa mwanasoka matata wa Chelsea, Branislav Ivanovic alivunja bila kutarajia kombe la Russian Cup ambalo waajiri wake wa sasa Zenit St Petersburg walipokezwa baada ya kuwapepeta FC Khimki 1-0 kwenye fainali ya Julai 25, 2020 iliyopigiwa jijini Moscow.
Kombe liliponyoka mikononi mwa beki na nahodha huyo alipokuwa akilinyanyua juu kwa juu hewani. Lilidondoka chini baada ya takriban sekunde 30 pekee na kuvunjika vipande vipande.
Ililazimu wanasoka wa St Petersburg kusitisha sherehe yao kwa muda na kujaribu kuliunganisha upya kombe hilo lakini juhudi zao ziliambulia pakavu.
Jumbe za kumdhihaki Ivanovic na wenzake zilimiminwa na wapinzani pamoja na mashabiki wa washindani wao kwenye mtandao wa Twitter pindi baadaye.
Martin Ogilvie alisema: “Kuvunjika kombe ni jambo ambalo sijawahi kuliona katika historia ya soka. Sidhani ni jambo la busara. Wavihifadhi vipande vivyo hivyo kabatini mwao.”
“Sergio Ramos wa Real Madrid aliwahi pia kufanya hivyo akiwa juu ya basi lao wakati wa gwaride la heshima la kusherehekea ubingwa wao wa Klabu Bingwa Ulaya mnamo 2016-17,” akasema shabiki mwingine wa FC Khimki aitwaye George.
“Hakuwa na nguvu za kunyanyua taji hilo. Alionekana kuzidi na uzito tangu mwanzo. Huenda kombe hilo lilitengenezwa kwa nanga!” akaandika Jack Gregory.
Ivanovic, 35, aliingia katika sajili rasmi ya Zenit St Petersburg mnamo 2017. Alihudumu kambini mwa Chelsea kwa kipindi cha miaka tisa kati ya 2008 na 2017 na aliwahi kuwaongoza miamba hao wa soka ya Uingereza kunyanyua taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2012. Beki huyo alisajiliwa na Chelsea kutokea Lokomotiv Moscow kwa kima cha Sh1.3 bilioni.
Video za kuonyesha kombe likiponyoka mikononi mwa Ivanovic kisha kuanguka sakafuni kutoka urefu wa futi saba na nusu na kuvunjika vipande vipande zimefutwa mitandaoni na kikosi cha Zenit St Petersburg kinachojiandaa kwa sasa kumsajili beki wa Liverpool, Dejan Lovren.
Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure.
Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.
Ernest
Hii ni bahati mbaya tuu ukiangalia jinsi lilivyomponyoka hakuweza ata kulizuia na pia litokee wazo la kubadilisha aina ya makombe sasa.
mwajumah
Ni bahati mbaya limemdondoka bila ya kutalajia#Meridianbettz
Sadick
Ni jambo la kushitua unapotarajia furaha unaishia majonzi na majuto. Nadhani alikuwa na furaha iliyopitiliza hivyo kukosa umakini#meridianbettz
aisha
hiyo ni bahati mbaya jamani kwa jinsi walivyopigania ubigwa pole sana kaka ivanovic kwa kuvunja kombe kwa bahati mbaya
Magdalena
Bahati mbaya tu hutokea bila ya matarajio
Latifa juma mohamed
Nadhani ni bahati mbaya
Ester jackson
Nadhani sio kukusudia inawezekana alikuwa na furaha sana mpaka kutokea tendo hilo ninavyo vikiri kwa kuwa jambo hili huwa lishatokea zaidi ya Mara tatu wanao andaa makombe wakebadilisha kidogo matirio yao au kuongeza ujuzi ili ikitokea kama hivi liwe na uimara zaidi.asante kwa nakala meridian
Fatina
Furah ikizidi m2 unaweza kufanya chochote ni bahat mbay 2 imetokea!!
Khadija
Nadhani hata mwenyewe hakutarajia kama itatokea hivo ni bahati mbaya sana#meridianbettz
felister
hii inaitwa ajali kazini
Lydia Emmanuel Magoti
Pole Sana lvanovic wanasemaga ajali kazn ajakusudia
Mwanahamisi
Nadhani ni bahati mbaya
Isaya massawe
Atakua ameacha simanzi kwa klabu yake
Venerose
Pole sana ajali haina kinga
Theckla
Habari mbaya sana
marry
ajal kazini
Adelta
Nadhani Ni ajali kazini
Tatu
Furaha ikizidi sana mwisho huwa uzuni
Salma ngende
Dah inaasikitisha
Furahav
Kawaida tu,
devotha
daah hii ilikua ni bahati mbaya
Neema juma
Tuseme bahati mbayaaa
Gabriel
Safi
Adelta
Nadhani Ni ajali kazini
Genia Sikaluzwe
Hii ni bahati mbaya
lombo
duuh hatar San ajar kazn
Asia Abdy
Hakukusudia
Hope mwaikuka
Aikua kusud so tusilaum
sabrina
Bahati mbaya
Povel
Duh majanga kwl kwl
Issa
Ivanovic bonge la mchezaj mahiri sana
Amiri Kayera
Duh majanga
Shafii
Bahati mbaya.
Samiah
Nibahati mbaya
farida ahmadi
Hii nouma Sana
caroline
jamani bahati mbayaaaaa
warda
Ilikuwa mikosi balaa#Meridianbettz
Zeiyana
Mungu anamajaribu yake haikua kwa kukusudia kwake wafaham ivo.
tumaini
Maoni:Duuuu hatari
Janeflora malisa
Bahat mbaya
David Pere
Amefanya kusudii kulivunjaa