Mshambuliaji wa Tottenham Spurs Harry Kane amempita Thierry Henry na kuwa mfungaji bora katika Ligi ya Primia kwenye Dabi ya London ambapo amefunga bao kwa mkwaju wa penati hii leo dhidi ya Arsenal.
Nahodha huyo wa Uingereza amefikisha bao moja mbele ya nguli wa The Gunners Henry, na sasa amefunga mabao 14 ya Primia Ligi dhidi ya Arsenal. Kane alikuwa tayari ni mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza kwenye Dabi ya London ya Kaskazini, na sasa amefunga penati saba dhidi ya The Gunners kwenye mechi ya ligi kuu.
Ni Alan Shearer pekee, ambae alifunga mikwaju saba dhidi ya Everton, ambaye amefunga penati nyingi dhidi ya mpinzani mmoja katika historia ya Ligi kuu ya Uingereza, Wakati huo huo, bao la Kane pia limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kupachika bao la ugenini kwa karne moja kwenye mashindano hayo.