Harry Kane mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza klabu ya Tottenham Hotspurs amechukizwa na kitendo cha kibaguzi kilichofanywa kwa mchezaji mwezaje wa klabu hiyo Richarlison raia wa Brazil.
Harry Kane amechukizwa na kitendo alichofanyiwa Richarlison wakati akiitumikia timu yake ya taifa mwanzoni mwa wiki hii na kusema hakikubaliki huku akitoa wito kwa shirikisho la soka duniani FIFA kuhakikisha wanachukua hatua stahiki.
Richarlison alirushiwa ndizi wakati anasherehekea bao wakati timu yake ya taifa ya Brazil ilipokua ikicheza na timu ya taifa ya Tunisia na kuibuka na ushindi wa mabao matano kwa moja katika mchezo uliopigwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa siku ya jumanne.
Mchezaji huyo wa Brazil alijitokeza kwenye mitandao yake ya kijamii na kutaka adhabu kali ichukuliwe kwa waliohusika na kitendo hicho huku watu wengine wakiunga mkono kama nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United Rio Ferdinand.
Ndipo Harry Kane alipoongeza nguvu na kulitaka shirikisho kuongeza nguvu dhidi ya vitendo vya ubaguzi “Ilikua ya kuakatisha tamaa sana sijapata nafasi ya kuona lakini naongelea kitendo alichofanyiwa Richy kwenye mchezo dhidi ya Tunisia.
“Nadhani FIFA wamesema watachunguza na kubaini kilichotokea,ila kikawaida kitendo hicho hakikubaliki”alisema Kane
“Nadhani sisi kama wachezaji tunapambana kuhakikisha ubaguzi unakwisha, lakini FIFA wana nguvu kuhakikisha jambo hili linapatiwa ufumbuzi au kuchukuliwa hatua stahiki”.