Lucas Moura Mchezaji wa timu ya Tottenham anaamini mchezaji mwenzake wa klabu hiyo Heung Ming Song ataendeleza moto wake wa kufumania nyavu kuelekea dabi ya London Kaskazini hapo kesho.

lucas mouraSon alishindwa kuonesha makali na kufunga magoli katika mechi za awali za ligi kuu nchini Uingereza kabla ya kufunga magoli matatu katika mchezo dhidi ya Leicester kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Kabla ya Son hakuficha kusikitishwa na kiwango chake katika timu hiyo, huku akikatishwa tamaa na uwezo wake mpaka ikafika hatua akidhani anawakatisha tamaa na wenzake nyota huyo ambaye alikua mfungaji bora wa ligi kuu Uingereza kwa msimu uliomalizika.

“Ni juu yake. Kuishusha timu ni maneno makali sana sichambui mabao au nambari tu, bali naona kile kijana anachangia kwa timu katika dakika 90 za mchezo”alisema Lucas Moura

Lucas moura anaeleza “Hata straika anaweza kuchangia sana katika mchezo lakini asifunge wala kutoa pasi bao, Son ni mtu mahiri sana, anasumbua sana mabeki wa timu pinzani. Anakimbia kila mara, na hilo linafungua nafasi nyingi kwa washambuliaji wengine”

lucas moura“Kwahiyi, ni mtu muhimu sana hata asipofunga bao bila shaka kuna presha binafsi inamkabili, nafikiri anajipa presha kubwa”.Moura anaendelea kueleza ni namna gani walikua wanamuona mchezaji mwenzao huyo alikua ana shauka ya kufunga bao la kwanza msimu huu baada ya kua hajafunga katika michezo kadhaa.

Moura anaeleza kua wachezaji wote walifurahia kufunga kwake kwakua ni mchezaji anaependwa na wachezaji huku yeye mwenyewe akiwa ni rafiki mkubwa wa Son akisema ni miongoni mwa marafiki wakubwa ambao soka imempatia.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa