Marcus Rashford na Anthony Martial wachezaji wa klabu ya Manchester United wanaelezwa kuna uwezekano wa kuikosa dabi ya Manchester kati yao na mahasimu wao klabu ya Manchester City siku ya jumapili.

marcus rashfordAnthony Martial amekua akisumbuliwa na majeraha katika kipindi cha kujianda na msimu lakini alipona majeraha yake na kurejea katika mchezo wa dhidi ya Liverpool lakini kuanzia ule mchezo alipata majeraha tena.

Kwa upande wa Marcus Rashford alicheza kwa kiwango cha hali ya juu katika michezo minne ya mwisho ya klabu hiyo lakini kuna taarifa ya kupata majeraha madogo na kuleta mashaka kuelekea dabi ya jiji la Manchester siku ya jumapili.

Marcus Rashford na Anthony Martial wamekua miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Man United chini ya mwalimu Eric ten Hag bahati mbaya Martial amekua mtu wa kupata majeraha mara kwa mara kwa sasa jambo ambalo linampasua kichwa mwalimu huyo.

marcus rashfordWachezaji hao inaelezwa wana hatihati ila hakuna taarifa rasmi kwamba wachezaji hao watakosekana katika mchezo hii ni kutokana na majeraha yao na kutokuonekana katika kiwanja cha mazoezi pamoja na wenzao.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa